• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 6 wauawa katika mlipuko wa bomu la ardhini Somalia

    (GMT+08:00) 2017-10-23 09:52:39

    Watu wasiopungua 6 wameuawa katika eneo la Shabelle ya kati nchini Somalia, baada ya basi dogo kukanyaga bomu lililotegwa ardhini.

    Waziri wa habari wa jimbo la Hirshabelle Bw. Mahad Hassan amesema mlipuko huo ulitokea kwenye kijiji cha Daniga, kilomita 15 magharibi ya mji wa Bal'ad baada ya basi moja lililobeba mboga kutoka Afgoye na kuelekea Bal'ad kukanyaga bomu lililotegwa kando ya barabara.

    Mkazi mmoja wa eneo hilo amesema wanawake wanne, dereva na kondakta waliokuwepo kwenye basi hilo waliuawa katika mlipuko huo.

    Kundi la Al Shabaab ambalo hufanya mashambulizi kama hayo mara kwa mara halijatoa taarifa yoyote kuhusu shambulizi hilo, ambalo limetokea baada ya shambulizi kubwa mjini Mogadishu kusababisha vifo vya watu 350.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako