• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China ya zama hizi yaweza kutoa mchango kwenye maendeleo ya dunia

    (GMT+08:00) 2017-10-23 16:41:35

    Ripoti iliyotolewa na rais Xi Jinping wa China kwenye mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China imesema, Ujamaa wenye umaalumu wa China umeingia katika kipindi kipya, na China imeingia kwenye kipindi cha kihistoria na kuwa na ushawishi zaidi duniani. Lakini je China ya zama tulizonazo itakuwa na ushawishi gani kwenye hali ya dunia? Fadhili Mpunji ana maelezo zaidi.

    Mwezi Agosti mwaka huu, kampuni ya utafiti wa masoko ya Ufaransa ya Ipsos ilifanya utafiti wa maoni ya umma kwenye nchi 26, ikiwa ni pamoja na China, Marekani, Uingereza na Japan. Utafiti huo umeoneysha kwamba, asilimia 87 ya wachina wana matumaini mazuri kwa maendeleo ya siku za baadaye ya China, na kuwa kwenye nafasi ya kwanza kwenye utafiti huo. Matokeo hayo yameongeza imani kwa hali ya maendeleo ya dunia inayokabiliana na matatizo mengi.

    Mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti wa Mashariki ya Mbali ya Russia Bw Sergey Luzianin amesema, China imepata mafanikio katika uvumbuzi wa maendeleo ya uchumi na ushirikiano wa kimataifa. Mpango uliotolewa na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kwenye mkutano huo umetoa mfano wa kuigwa kwa maendeleo ya nchi mbalimbali.

    "mafanikio ya China si kama tu yanasaidia maendeleo ya China yenyewe bali pia yametoa mfano wa kuigwa na uzoefu kwa nchi mbalimbali katika kutimiza uchumi wa kisasa."

    Waziri wa habari na mawasiliano wa Zimbabwe Bw Simon Moyo amesema, uzoefu wa China pia utasaidia kwenye harakati za kupambana na rushwa.

    "tunapongeza mafanikio makubwa ya Chama cha kikomunisti cha China katika kupambana na ufisadi. Nchini Zimbabwe, sisi pia tunapambana na ufisadi, lakini hii si kazi rahisi. Tunapaswa kuiga uzoefu wa China hasa kutoka kwa maofisa wanaoshughulikia kazi hii."

    Mkuu wa uhusiano wa kimataifa wa chama cha kikomunisti cha Ufaransa Bibi Lydia Samarbakhsh, anaona mkutano huo umeonesha nia ya China kuwajibika na kupenda kusaidia usimamizi wa dunia na maendeleo ya amani.

    "hivi sasa, tofauti kati ya nchi mbalimbali zinaendelea kuongezeka. Lakini mapendekezo yaliyotolewa na China kuhusu kushughulikia mmabo ya dunia na maendeleo ya amani yatashirikisha nchi hizo. Hakuna mtu mwenye uwezo wa kuishi kwa heshima bila kutegemea watu wengine. Hivyo, sisi sote tunapaswa kufanya juhudi kwa pamoja kuondoa tofauti za kisiasa na kubadilisha hali mbaya, ili kuboresha maisha ya watu wote na kupata uwezo wa kukidhi mahitaji ya wananchi wote katika afya, elimu, usafiri, makazi nk."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako