• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Taasisi ya sayansi ya China yakuza mpunga wa aina mpya wenye urefu wa mita 2.2

  (GMT+08:00) 2017-10-23 18:21:28

  Idara ya kilimo katika ukanda wa nusu tropiki ya Taasisi ya sayansi ya China imekuza mpunga wa aina mpya ambao urefu wake unaweza kufikia mita 2.2.

  Mtafiti wa idara hiyo Bw. Xia Xinjie amefahamisha kuwa mpunga huo unafanya usanisinuru kwa ufanisi mkubwa zaidi kuliko mpunga wa kawaida kwa asilimia 50, kwa wastani mmea mmoja una machaka 40, mpunga unaokua kwenye chaka moja unaweza kufikia zaidi ya 500, na uzalishaji wa michele unaweza kufikia tani 12 kwa hekta.

  Mpunga huo una shina nene lenye kipenyo cha milimita 18.5, na majani yake yanafunikwa na nta, hivyo ni vigumu kuangushwa na upepo, unakinga wadudu na mafuriko.

  Bw. Xia amesema mpunga huo umekuwa wenyewe kwa kutumia teknolojia mbalimbali mpya zikiwemo kuchochea mabadiliko ya mpunga, kukuza mpunga chotara kwa kutumia mpunga pori, na kuchagua aina nzuri za mpunga kwa mujibu wa alama za molekuli.

  Mkurugenzi wa idara hiyo Bw. Wu Jinshui amesema mpunga huo mrefu unapandwa kwenye mashamba yenye maji ya kina, hivyo utaweka mazingira mazuri kwa ufugaji wa samaki mashambani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako