• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanaakiolojia wagundua sanduku la chakula lenye historia ya miaka 4000

    (GMT+08:00) 2017-10-23 18:21:45

    Je, watu wa kale walipeleka chakula gani walipokwenda porini? Wanaakiolojia wamepata jibu la swali hilo baada ya kugundua sanduku la chakula lenye historia ya miaka 4000.

    Wanaakiolojia wa Uswisi wamegundua sanduku la chakula la mbao, upinde, kamba na vitu vya ngozi chini ya mwamba mkubwa katika mlango wa mlima wa Lotschen wenye mita 2700 wa eneo la Alps nchini humo.

    Baada ya kupima Carbon-14 kwenye vitu hivi, wanaakiolojia wamegundua kuwa vitu hivi vilimilikiwa na wawindaji au wafugaji wa miaka 4000 iliyopita. Huenda waliacha vitu hivi walipokimbia upepo au theluji chini ya mwamba mkubwa.

    Sanduku la chakula lenye umbo la duara lilitengenezwa kwa mbao za msonobari na willow, na bado kuna mabaki ya vyakula kwenye sanduku hilo. Wanaakiolojia wamegundua kuwa mabaki hayo ni unga wa ngano na shayiri.

    Wanaakiolojia wamesema watu wa kale huenda walichanganya unga na maji au maziwa walipokula, kwa sababu unga ni mwepesi zaidi na ni rahisi kuumeza.

    Wanaakiolojia wamesema mabaki hayo ya kihisotira yamethibitisha kuwepo kwa wawindaji katika zama ya shaba nyeusi katika eneo hilo. Siku hizi mlango wa mlima Lotschen bado ni eneo la uwindaji lenye kondoo wa buluu na mbuzi mwitu wengi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako