• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mpasuko wazidi kuwagawa wananchi wa Kenya ikiwa inaelekea kwenye uchaguzi wa marudio

    (GMT+08:00) 2017-10-23 19:44:26

    Msuguano kati ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na kiongozi wa upinzani Raila Odinga unaendelea kuigawa Kenya wakati ambapo uchaguzi wa marudio unatarajiwa kufanyika Alhamis wiki hii.

    Viongozi hao wanashikilia misimamo yao kwenye uchaguzi, ambapo rais Kenyatta anasema uchaguzi lazima uendelee ili nchi iweze kusonga mbele huku Odinga akidhamiria kusitisha uchaguzi huo, na kusisitiza kuwa hakutakuwa na uchaguzi Oktoba 26. Viongozi hao wamekuwa wakirushiana maneno katika siku zilizopita, rais Kenyatta akimshutumu Odinga kutaka kukawilisha maendeleo ya nchi kwa kukataa marudio ya uchaguzi. Wakati huohuo Odinga anamshutumu Kenyatta kwa kujilazimisha kwa wakenya kupitia uchaguzi usio halali na kuitisha maandamano dhidi ya uchaguzi huo.

    Mpasuko huo umewafanya wakenya kuhofia na kutojua kitakachotokea baada ya uchaguzi wa marudio siku ya Alhamisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako