• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UN na AU wahimiza amani wakati wa marudio ya uchaguzi Kenya

    (GMT+08:00) 2017-10-24 09:22:59

    Umoja wa Afrika na Umoja wa mataifa wamewahimiza wanasiasa wa Kenya kutatua mvutano kati yao kwa mujibu wa sheria, huku mashirika ya kijamii na wapinzani wakitoa wito wa kusitishwa kwa uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika alhamisi.

    Taarifa ya pamoja iliyotolewa jumapili usiku na katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Bw Moussa Faki Mahamat imesema viongozi wote wanafaa kuhakikisha kwamba uchaguzi unafanyika ndani ya mfumo wa kisheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako