• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bibi May asema Uingereza na EU wapo kwenye hatua ya mwisho ya kuafikiana kuhusu haki za raia

    (GMT+08:00) 2017-10-24 09:27:05

    Uingereza na Umoja wa Ulaya zipo kwenye hatua za mwisho za kutatua hatma ya mamilioni ya raia wa Umoja wa Ulaya wanaoishi nchini Uingereza.

    Waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May amesema hayo akiwasilisha ripoti bungeni ambapo nchi hiyo inatarajiwa kujitoa kwenye umoja huo Machi 2019. Akiongea kuhusu haki za raia, Bibi May amesema pande zote mbili zina malengo sawa ya kulinda haki za raia wa Umoja wa Ulaya waishio Uingereza, na Waingereza waishio kwenye nchi za Umoja wa Ulaya.

    Bibi May pia amesisitiza kuwa hakutakuwa na uzio kwenye mpaka kati ya Jamhuri ya Ireland na Ireland Kaskazini, na kuongeza kuwa utaratibu wa usafiri wa kawaida kati ya Uingereza na Ireland utaendelea. Amewaambia wabunge kuwa katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya uliofanyika wiki iliyopita, wajumbe walikubali kuanza maandalizi ya kuhamishia mazungumzo kwenye biashara na hatma ya uhusiano wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako