Katika miaka mitano iliyopita Chama cha Kikomunisti cha China kimeonyesha ushupavu na dhamira na kutumia nguvu kubwa katika kusimamia mienendo ya wanachama, kupambana na ufisadi, kusimamia nidhamu ya chama na kuwaunganisha wanachama na wananchi, hatua ambazo zimeimarisha msingi wa utawala wa chama.
Jumuiya ya kimataifa inaona juhudi za chama hicho kuongeza nguvu katika kukamilisha mfumo wa sheria na kanuni za chama, na kujijenga uwezo wa utawala kumekuwa msingi kwa China kuwa na utulivu, maendeleo na ustawi.
Katibu mkuu wa muungano wa vyama tawala wa Kenya Jubilee Bw. Raphael Tuju anaona kuimarisha usimamizi kwa wanachama na kuhakikisha utiifu wa wanachama ni hatua muhimu zinazochukuliwa na chama cha kikomunisti kudumisha sifa zake.
Gazeti la Independent la Russia linaona juhudi za bila kusita zinazofanywa na chama cha CPC katika kupambana na ufisadi zinalenga kuleta uwiano kati ya uchumi wa soko huria na mfumo wa ujamaa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |