Bw. Abadi amesema hatua zinazochukuliwa na serikali ya Iraq huko Kirkuk, ni kupanga upya na kutekeleza madaraka ya utawala, ambazo ni hatua halali kwa mujibu wa katiba na sheria, na kwamba serikali kuu haitaki kupambana na upande wowote wa Iraq.
Habari nyingine zinasema waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergey Lavrov jana huko Moscow alipokutana na waziri wa mambo ya nje wa Iraq Bw. Ibrahim al-Jaafari, alisema Russia inaheshimu ukamilifu wa ardhi wa Iraq na Russia inatoa wito wa masuala yote kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo, pia alisistiza kuwa wakati wa kuhimiza utatuzi wa kisiasa wa migogoro ya kikanda, ni muhimu kuzuia kutenga au kuweka mipaka kwa kufuata dini au makabila.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |