Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha kikomunisti cha China umefungwa leo hapa Beijing, ambapo Kamati kuu ya awamu mpya ya Chama cha kikomunisti cha China na kamati ya ukaguzi wa nidhamu ya kamati kuu mpya ya chama zimechaguliwa. Mkutano huo pia umepitisha uamuzi kuhusu ripoti ya kamati kuu ya 18 ya chama, uamuzi wa ripoti ya kazi ya kamati ya ukaguzi wa nidhamu, na uamuzi wa marekebisho ya katiba ya chama.
Mkutano huo umekubali kuiweka fikra ya Xi Jinping kuhusu ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya kwenye katiba ya chama, ikiwa pamoja na Umax-Lenin, Fikra Mao Zedong, Nadharia ya Deng Xiaoping, Fikra muhimu ya "Uwakilishi mtatu" na Wazo la kujiendeleza kwa njia ya kisayansi, na kuichukulia kuwa mwongozo wa utekelezaji wa chama.
Katibu mkuu wa chama hicho Bw. Xi Jinping ameendesha ufungaji wa mkutano huo, uliohudhuriwa na wajumbe na waalikwa wengine wapatao 2336.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |