• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kujenga mfumo wa uchumi wa kisasa kutaongoza uchumi wa China uendelezwe vizuri kwa utulivu na kupata maendeleo endelevu

    (GMT+08:00) 2017-10-24 18:13:13

    Ripoti ya mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China imetangaza kuwa Ujamaa wenye umaalumu wa China umeingia kwenye Zama mpya. Ripoti hiyo pia imesisitiza kujenga mfumo wa uchumi wa kisasa kwa kuimarisha mageuzi ya muundo wa utoaji wa bidhaa na huduma, kuharakisha kujenga nchi yenye uvumbuzi, kutekeleza mkakati wa kusitawishavijiji na maendeleo ya uwiano wa kikanda, kuharakisha kukamilisha utaratibu wa uchumi wa soko huria wa kijamaa na kusukuma mbele hali mpya ya kufungua mlango. Wajumbe wa mkutano huo wanaona, kujenga mfumo wa uchumi wa kisasa utasaidia maendeleo endelevu ya uchumi wa China.

    Ripoti hiyo imesisitiza umuhimu wa kuharakisha maendeleo ya kiviwanda, kusukuma mbele ushirikiano kati ya uchumi na mtandao, data kubwa za kitarakimu, na kuongeza uwezo wa akili zisizo za kibinadamu. Mkuu wa idara ya kompyuta zenye uwezo mkubwa ya China mjini Tianjin Bw. Meng Xiangfei anasema,

    "Tumeanzisha utafiti wa kompyuta mpya yenye uwezo wa ExaFLOPS. Pia tunafanya utafiti wa kujenga mfumo wa ushirikiano wa kompyuta yenye uwezo mkubwa, data kubwa za kitarakimu, na uwezo wa akili zisizo za kibinadamu. Licha ya hayo, tutajitahidi kujenga mfumo wa data kubwa za tarakimu kuhusu matanuri ya chuma na chuma cha pua, na kujenga migodi ya kidigitali."

    Kilimo, vijiji na wakulima ni masuala yanayotiwa mkazo na serikali ya China. Katibu wa Kamati ya chama ya kijiji cha Beidouxi Bibi Liang Jinhua anasema,

    "Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kijiji chetu kinapaswa kujengwa kuwa kijiji chenye ustawi na neema, mazingira mazuri yanayofaa kwa kuishi yenye ustaarabu kwenye jamii. Lengo hili ni matarajio ya wanakijiji wote, pia ni matumaini tutakayotimiza."

    Hivi sasa, China inaendelea kuwa nchi ya pili ya utoaji mkubwa wa uchumi duniani. China inapaswa kuzidi kuendeleza mfumo wa kufungua mlango na kukaribisha zaidi makampuni ya nje ili kumaliza kujenga mfumo wa uchumi wa kisasa. Naibu mkurugenzi wa idara ya mageuzi na maendeleo ya China Bw. Ning Jizhe anasema,

    "China inapanga kurahisisha ruhusa ya makampuni ya nje kuingia kwenye soko la China. Makampuni hayo yakipata ruhusa ya kuingia, yatatambuliwa kama kampuni ya ndani. Makampuni yoyote yaliyosajiliwa nchini China, yote yatatendewa kwa usawa. Katika kazi ya kurahisisha uwekezaji, China itashikilia kutekeleza utaratibu mpya wa kurekodi taarifa za kuanzishwa na kurekebishwa kwa makampuni ya nje badala ya kuidhinisha."

    Ripoti hiyo pia imesistiza kusukuma mbele maendeleo ya makampuni ya kiserikali na kuunga mkono maendeleo ya makampuni binafsi. Mwenyekiti wa Kamati ya usimamizi wa benki ya China Bw. Guo Shuqing anasema,

    "China inapaswa kuendelea kuboresha kazi ya utoaji huduma na kujitahidi kuunga mkono benki kusaidia kazi ya kukusanya mitaji kwa makampuni madogomadogo, kazi za kilimo na vijijini, ili kuondoa umaskini. Hali kadhalika, kuendelea kuunga mkono ujenzi wa miundo mbinu na makazi bora."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako