• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNICEF yatoa wito kuzitaka nchi za kati na magharibi mwa Afrika kuchukua hatua kuzuia ndoa za watoto

    (GMT+08:00) 2017-10-24 18:36:38

    Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limetoa ripoti ikisema ndoa za utotoni bado zinatokea mara kwa mara katika nchi za kati na magharibi mwa Afrika

    Ripoti inaonesha kuwa ndoa za utotoni katika kanda hiyo zimepungua ikilinganishwa na miaka 20 iliyopita, lakini zinapungua polepole. Hivi sasa robo ya wasichana wanafunga ndoa kabla ya umri wa miaka 18, na miongoni mwao theluthi moja hawajafikia umri wa miaka 15.

    Ripoti hiyo inasema miongoni mwa nchi 10 zenye ndoa nyingi zaidi za watoto duniani, 6 ziko kati na magharibi mwa Afrika, ambazo ni pamoja na Niger, Afrika ya Kati, Chad, Mali, Burkina Faso na Guinea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako