• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shirika la afya duniani latoa mwito wa kuondoa ubaguzi kwa wagonjwa wa Ukimwi

  (GMT+08:00) 2017-10-24 20:41:43

  Mkurugenzi wa shirika la afya duniani WHO Bw. Tedros Adhanom Ghebreyesus jana kwenye makao makuu ya shirika hilo alikutana na wajumbe wa wanafunzi wa China walioambikizwa virusi vya Ukimwi. Amewataka watu duniani waondoe ubaguzi kwa wagonjwa wa Ukimwi, pia amesifu juhudi za vijana wa China katika kuwafuatilia wagonjwa wa Ukimwi na kuondoa ubaguzi dhidi yao.

  Wanafunzi hao wa China wameishukuru nchi yao kwa kutoa matibabu ya ugonjwa wa Ukimwi na fursa za kupata elimu. Wamesema wanaweza kuishi na kusoma kama watu wengine, pia wanaweza kutoa mchango kwa jamii kwa kupitia juhudi zao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako