• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UN atoa wito wa juhudi za pamoja kukabiliana na changamoto duniani

    (GMT+08:00) 2017-10-25 09:45:47

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Antonio Guterress ametoa hotuba ya kuadhimisha Siku ya Umoja wa Mataifa, akitoa wito kwa nchi zote kushirikiana katika kukabiliana na changamoto duniani.

    Bw Guterress amesema hivi sasa kuna changamoto nyingi zinazowakabili binadamu, ikiwa ni pamoja na kutokuwepo kwa usawa, matishio ya usalama na hali mbaya ya hewa. Ametoa wito wa kujenga dunia yenye haki na amani, na maendeleo endelevu.

    Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa yalifanyika jana jijini Beijing, chini ya kauli mbiu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu. Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini China Bw Nicholas Rosellini alihudhuria maadhimisho hayo na kuhimiza utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako