• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Putin asema ufufukaji wa uchumi wa Russia umeonesha dalili za utulivu

    (GMT+08:00) 2017-10-25 10:34:50

    Rais Vladimir Putin wa Russia amesema, uchumi wa Russia umeondokana na hali ya kudidimia huku ufufukaji ukionesha dalili za utulivu.

    Rais Putin amesema kuanzia mwezi Januari hadi Septemba mwaka huu, thamani ya jumla ya pato la taifa limeongezeka kwa asilimia 1.8, ikiwa imeongezeka kwa miezi 12 mfululizo, ambapo sekta zinazokua kwa kasi zaidi ni utengenezaji wa magari, dawa, kemikali, vyakula na vifaa vya kielektroniki.

    Rais Putin pia amesema, katika robo tatu za mwanzo za mwaka huu, uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nchi za nje katika sekta zisizo za kifedha nchini Russia umeongezeka mara 2.5 hadi kufikia dola bilioni 23 za kimarekani, ambazo ni juu zaidi katika miaka minne iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako