• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Kenya lawaua wapiganaji wanne wa Al-Shabaab mkoa wa pwani

    (GMT+08:00) 2017-10-25 10:59:37

    Msemaji wa jeshi la Kenya KDF Bw. David Obonyo amesema, askari wa jeshi la Kenya wameshambulia kambi ya kundi la Al-Shabaab iliyoko huko Lamu na kuwaangamiza wapiganaji wanne wa kundi hilo.

    Bw. Obonyo amesema, shambulizi hilo limefanywa katika eneo la Mararani katika kaunti ya Lamu, na kukamata silaha na chakula chao.

    Amesema inaaminika kuwa magaidi kadhaa walikimbia wakiwa na majeraha. Kambi hiyo inadaiwa kutumiwa kama kituo cha mafunzo na kufanya operesheni cha magaidi, ambao wamefanya mashambulizi hivi karibuni katika eneo hilo nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako