• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa Jamhuri ya Kongo nchini China asema China imetoa mfano wa kuigwa katika kuondoa umaskini

    (GMT+08:00) 2017-10-25 18:02:01

    Balozi wa Jamhuri ya Kongo nchini China Bw. Daniel Owassa amesema, tangu mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha kikomunisti cha China ufanyike miaka mitano iliyopita, China imepata mafanikio makubwa katika kuondoa umaskini na kutoa mfano wa kuigwa kwa nchi mbalimbali duniani. Pili Mwinyi ana maelezo zaidi.

    Ripoti ya mkutano huo imesema, katika miaka mitano iliyopita, China imesaidia watu milioni 60 kuondokana na umaskini. Kiwango cha umaskini kimepungua kutoka asilimia 10.2 hadi 4. Akiwa ni balozi wa Jamhuri ya Kongo nchini China, Bw. Owassa anathibitisha maendeleo ya kila siku ya China katika kuondoa umaskini. Anasema,

    "Nchi nyingi zinatarajia misaada kutoka benki ya dunia au Shirika la fedha duniani kuzisaidia kuondoa umaskini. Lakini, China imetegemea nguvu yake yenyewe kutatua suala hili. Hivyo, imezifundisha nchi mbalimbali hasa nchi za Afrika namna ya kuondoa umaskini."

    Ripoti ya mkutano huo pia imesema, maendeleo ya uchumi wa China yamebadilisha hali kutoka kuzingatia kasi hadi kutilia maanani ubora. Bw. Owassa amesema, katika miaka ya hivi karibuni, China imejitahidi kuhimiza maendeleo ya uchumi na kupata mafanikio makubwa. Anaona, maendeleo ya uchumi ya China yana mustakabali mzuri.

    "Baadhi ya watu wanaona, upungufu wa ongezeko la uchumi wa China ni kama balaa. Lakini tunapaswa kuona, ongezeko hilo linatakiwa kutokana na kiasi kikubwa zaidi cha utoaji wa uchumi. Ongezeko hilo la China ni mafanikio makubwa kwa China. Hivi sasa, ni vigumu kwa baadhi ya nchi kudumisha ongezeko la asilimia 5 la uchumi, lakini China bado inaendelea kudumisha ongezeko la asilimia zaidi ya 6."

    Katika miaka ya hivi karibuni, ushirikiano wa kiviwanda umekuwa muhimu zaidi kati ya China na Afrika. "Kuhimiza ushirikiano wa kiviwanda wa kimataifa" pia imeandikwa kwenye ripoti hiyo. Akizungumzia suala hili, Bw. Owassa amesema, ushirikiano wa kiviwanda umetoa fursa mpya kwa ushirikiano kati ya China na Afrika. Ikiwa ni nchi ya kwanza kutekeleza ushirikiano huo, Jamhuri ya Kongo imepata manufaa mengi.

    "Katika mkutano wa wakuu wa Baraza la Ushirikiano la China na Afrika, rais Xi Jinping wa China ametoa mipango 10 ya ushirikiano kati ya China na Afrika, ikiwemo, ushirikiano katika sekta ya viwanda. Nchi yetu imenufaika kutokana na ushirikiano huo kwa kuanzisha eneo maalum la kiuchumi la Blackjack nchini humo."

    Ripoti ya mkutano huo pia imetaja kuongeza misaada kwa nchi zinazoendelea hasa nchi zilizoko nyuma zaidi kimaendeleo ili kusaidia kupunguza pengo la maendeleo kati ya kusini na kaskazini. Bw. Owassa amesema, China ilianza kutoa msaada kwa nchi zinazoendelea hasa katika kipindi chake kigumu. Hivi leo, China imepata maendeleo makubwa na kuendelea kusaidia nchi nyingine zinazoendelea. China ni miongoni mwa nchi chache tu zinazopenda kushauriana kuhusu matokeo mazuri ya maendeleo.

    "Ni jambo zuri kwa China kuendelea kuongeza misaada kwa nchi zinazoendelea. Si nchi zote zinapenda kuchukua hatua hiyo. Tumeona, baadhi ya nchi kubwa si kama tu hazipendi kutusaidia, bali pia zinapenda kujinufaisha. Katika ushirikiano wa kusini na kusini, China imefanya kazi kubwa kwa ajili ya maendeleo ya nchi zinazoendelea."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako