• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pakistan kufanya juhudi kuondoa nguvu za kigaidi

    (GMT+08:00) 2017-10-25 18:10:00

    Waziri mkuu wa Pakistan Bw. Shahid Khaqan Abbasi alipofanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Rex Tillerson ambaye yuko ziarani nchini humo, amesema Pakistan inafanya juhudi kuondoa nguvu za kigaidi nchini humo, na inatarajia kuimarisha ushirikiano na Marekani katika mambo ya usalama na uchumi.

    Kwenye mazungumzo hayo, Bw. Abbasi amemweleza Bw. Tillerson hatua na mchango wa Pakistan katika mapambano dhidi ya ugaidi, na hatua zilizochukuliwa na Pakistan katika kuhimiza utulivu wa Afghanistan na kanda hiyo.

    Bw. Tillerson amesisitiza kuwa Pakistan inatakiwa kuongeza nguvu ya kuondoa watu wenye silaha na magaidi nchini humo. Pia amesema kupambana na kundi la IS, kuondoa makundi ya kigaidi, na kujenga Afghanistan yenye amani na utulivu kunaendana na maslahi ya Marekani na Pakistan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako