• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bodi ya Kilimo Rwanda yapongezwa kwa kufanikisha kahawa ya Rwanda kuwa bora duniani

    (GMT+08:00) 2017-10-25 18:16:40
    Wadau katika sekta ya kahawa wanasema sababu ya kahawa ya Rwanda kufanya vizuri kimataifa ni kutokana na mikakati mipya iliyotekelezwa na Bodi ya Kitaifa Kilimo na mauzo ya nje nchini humo NAEB).

    Kahawa ya Rwanda ilishikilia nafasi ya pili duniani kwa ubora wiki mbili zilizopita jijini New York Marekani.

    Kahawa hiyo ilishinda washindani wengine wanane na kuchukua tuzo yay a kahawa bora zaidi "Best of the Best" kutokana na kahwa hiyo kuwa ya kipekee,iliyokolea,harufu nzuri na ubora.

    Kahawa ya Rwanda ilishindana na kahawa za Brazil,Colombia,Costa Rica,Ethiopia,Guatemala,India,Nicaragua na Honduras,nchi zinazojulikana kuwa wazalishaji bora wa kahawa duniani wakati wa tathmini ya Umoja wa Mataifa ya kahawa bora inayokuzwa katika nchi tisa duniani.

    Kahawa iliyoshindanishwa ni ile inayokuzwa eneo la Rusizi,Lisa na Mashesha ambayo ilichaguliwa miongoni mwa 27 bora duniani kutoka mavuno ya mwaka 2016/2017 katika nchi hizo tisa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako