• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiongozi wa Iran akataa kufanya mazungumzo kuhusu mpango wa kuendeleza makombora

    (GMT+08:00) 2017-10-26 09:04:34

    Kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amesisitiza kuwa Iran kamwe haitajadili kuhusu uwezo wake wa ulinzi, ukiwemo mpango wake wa kuendeleza makombora.

    Bw. Khamenei alisema hayo kwenye sherehe iliyohudhuriwa na makamanda wa jeshi la Iran. Amesema leo ugomvi na mataifa jeuri ni kutokana na nia yao ya kudhibiti eneo la mashariki ya kati, akiwalenga Marekani na washirika wake wa magharibi. Amesisitiza kuwa, ili kuhakikisha usalama wa Iran, uwezo wake wa ulinzi haujadiliki kamwe.

    Habari nyingine zinasema, baraza la juu la bunge la Russia jana lilitoa taarifa ikitoa mwito wa kulinda makubaliano ya pande nyingi kuhusu suala la nyuklia la Iran, huku rais Donald Trump wa Marekani akitishia kuyavunja.

    Wabunge wa Russia wanaona kuvunjika kwa makubaliano hayo kutahujumu juhudi za kutoeneza silaha za nyuklia na kuzuia masuala ya nyuklia yanayofanana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako