Kwa upande wake Rais Xi Jinping ametoa shukrani kwa salamu za pongezi za rais Trump, akisema China itashikilia njia ya kujiendeleza kwa amani, kuendelea kufuata mkakati wa kufungua mlango kwa nje, kupanua maslahi ya pamoja ya nchi mbalimbali, na kuhimiza uratibu na ushirikiano kati ya nchi mbalimbali.
Rais Xi amesisitiza kuwa China inaweka mkazo mkubwa katika kukuza uhusiano na Marekani kwenye msingi wa kuheshimiana na kunufaishana.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |