• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Gianluigi Buffon anafikiria kustafu soka baada ya Fainali za Kombe la Dunia

  (GMT+08:00) 2017-10-26 09:49:40

  Nahodha wa timu ya taifa ya Italia 'Azzuri', Gianluigi Buffon amesema anatarajia kustaafu soka baada ya kumalizika Fainali za Kombe la Dunia.

  Buffon alisema atabadili uamuzi wake endapo 'Kibibi Kizee' cha Turin klabu ya Juventus itakata tiketi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Nguli huyo alitoa kauli hiyo katika hafla ya utoaji tuzo ya mchezaji bora wa dunia iliyofanyika London, England ambapo aliibuka kipa bora duniani.

  Licha ya kucheza soka muda mrefu, kipa huyo mwenye miaka 39, hakuwahi kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na sasa anafikiria kutundika daluga.

  Buffon alisema ana ndoto ya kuipa Juventus ubingwa wa Ulaya baada ya kuipa Kombe la Dunia Italia ingawa alidai haitakuwa kazi rahisi kutokana na ushindani mkali kwenye Ligi Kuu Italia msimu huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako