• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu 32 wafariki dunia kwenye ajali ya moto nchini Indonesia

  (GMT+08:00) 2017-10-26 18:58:47

  Kiwanda cha fataki kilichopo mjini Tanggerang karibu na mji mkuu wa Indonesia kimeungua moto leo asubuhi, na kupelekea vifo vya wafanyakazi 32 na wengine 46 kujeruhiwa.

  Kwa mujibu wa afisa zima moto, Hanaf aliyekuwepo kwenye tukio, idadi ya waliokufa ni 30. Lakini afisa Doni Pratama amesema saa kadhaa baadaye, wafanyakazi wengine wawili wamepatikana wamekufa na sasa wanaendelea kutafuta kuona kama bado kuna miili ya wafanyakazi. Pratama na wafanyakazi wengine waokoaji wamepelekwa eneo la tukio kusaidia wafanyakazi wa zima moto na waokozi.

  Inadaiwa kuwa moto huo ulisababishwa na shoti ya umeme kwenye saketi uliosambaa kwenye bidhaa ambazo hazijahifadhiwa vizuri. Hata hivyo polisi wanaendelea na uchunguzi kujua chanzo halisi cha moto huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako