• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Fikra ya Xi Jinping kuhusu Ujamaa wenye umaalumu wa China yawekwa kwenye katiba ya Chama cha Kikomunisti cha China

  (GMT+08:00) 2017-10-26 19:55:05

  Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China umefungwa jana hapa Beijing. Mkutano huo umekubali kwa kauli moja kuiweka Fikra ya Xi Jinping kuhusu Ujamaa wenye umaalumu wa China kwenye katiba ya chama, na kuwaita wanachama wote wajifunze kwa nia imara zaidi na kwa hiari zaidi na kuitekeleza katika mchakato mzima wa ujenzi wa nchi na ujenzi wa chama katika siku za baadaye. Fikra ya Xi Jinping kuhusu Ujamaa wenye umaalumu wa China wa zama mpya imejibu kikamilifu namna Chama cha Kikomunisti cha China kinavyoshikilia na kuendeleza mada hii kubwa katika zama hizi, na kuanzisha hali na sura mpya ya Ujamaa wenye umaalumu wa China.

  Mkutano mkuu wa Chama wa awamu mbalimbali umerekebisha katiba ya chama na kuonesha umaalumu wa zama tofauti. Kwenye mkutano mkuu uliofungwa jana, chama tawala cha CPC kimetoa hoja muhimu ya kisiasa, kikisema migongano mikubwa kwenye jamii ya China imebadilika, na maendeleo ya Ujamaa wenye umaalumu wa China yameingia kwenye zama mpya. Naibu mkurugenzi wa Ofisi ya utafiti wa sera ya Kamati kuu ya chana Bw. Wang Xiaohui anaona kuwa, zama mpya zimetoa mada mpya, mada mpya zinaweza kusababisha nadharia mpya. Fikra ya Xi Jinping kuhusu Ujamaa wenye umaalumu wa China katika Zama mpya imejibu kwa uvumbuzi masuala makubwa yanayoikabili China katika zama mpya.

  "Mabadiliko ya kina katika hali ya ndani na nje na maendeleo kasi ya sekta mbalimbali za nchini China hayo yote yamesababisha fikra ya Xi Jinping kuhusu Ujamaa wenye umaalumu wa Cina wa zama mpya. Fikra hiyo imejibu kwa uvumbuzi mada muhimu katika uzoefu na zama hizi, yaani kushikilia Ujamaa wenye umaalumu wa China wa namna gani na kushikilia na kuendeleza kwa namna gani Ujamaa wenye umaalumu wa China."

  Tokea mkutano mkuu wa 18 ufanyike miaka mitano iliyopita, Chama cha kikomunisti cha China kimetoa hatua zipatazo 1500 za mageuzi na kupata mafanikio mkubwa, hasa katika hali ya kudidimia kwa uchumi wa dunia na masuala ya kimataifa kuendelea kuwa mabaya. Mafanikio hayo yote yanatokana na wanachama wa Chama cha kikomunisti wa China ambao Xi Jinping ni mwakilishi wao wanafuata maendeleo ya zama hizi na kuanzisha fikra ya Xi Jinping ya Ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya. Bw. Wang amesema, .

  "Bw, Xi Jinping ameeleza malengo ya jumla, majukumu ya jumla, mpango wa jumla, mikakati na mwelekeo wa maendeleo, njia ya kuendeleza, injini ya kuendeleza, hatua za kimkakati, hali ya nje na uhakikisho wa kisiasa kwa ajili ya kuongeza maana mpya ya kisayasi ya Ujamaa wenye umaalumu wa China, na kuongeza na kuendeleza mfumo wa nadharia ya Ujamaa wenye umaalumu wa China."

  Mkutano huo umethibitisha fikra ya uongozi ya zama mpya, pia umetoa majukumu ya kihistoria na matakwa mapya ya ujenzi wa chama. Mkuu wa kikundi cha kamati ya ukaguzi wa nidhamu ya kamati kuu ya chana Bw. Jiang Jinquan anaona kuwa, katika siku za baadaye, ujenzi wa Chama cha Kikomunisti cha China utaongozwa na ujenzi wa kisiasa ili kuendelea kuimarisha kazi ya kushughulikia matatizo ya chama kwa hatua kali.

  "Mpango wa ujumla ni kuufanya ujenzi wa kisiasa wa chama uwe uongozi wa kazi ya kusukuma mbele ujenzi wa siasa, ujenzi wa fikra, ujenzi wa oganezeshin, ujenzi wa mienendo na nidhamu, huku kufanya ujenzi wa utaratibu, kusukuma mbele mapambano dhidi ya ufisadi, kuongeza sifa ya ujenzi wa chama ili uwe kwenye safu ya mbele katika zama hizi, na kukijenga Chama cha kikomusti cha China kiwe chama tawala cha Umarx kinachoungwa mkono na wananchi, kinaweza kujirekebisha kijasiri, na kuwa na hamasa za kushinda taabu mbalimbali."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako