• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la usalama la UM latoa wito kwa serikali ya Iraq ifanye mazungumzo na jimbo la wakurdi

    (GMT+08:00) 2017-10-27 09:25:22

    Baraza la usalama la Umoja wa Matiafa limesema linafuatilia hali ya wasiwasi kati ya serikali kuu ya Iraq na jimbo la wakurdi, na kutoa wito kwa pande hizo mbili kufanya mazungumzo haraka iwezekanavyo.

    Mwenyekiti wa zamu wa baraza hilo kwa mwezi huu na balozi wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa Bw François Delattre, amesema Baraza la usalama la umoja huo limetoa wito kwa pande hizo mbili zifanye mazungumzo badala ya matumizi ya uguvu. Wajumbe wa baraza hilo wamesisitiza tena kuheshimu mamlaka, ukamilifu wa ardhi na umoja wa taifa la Iraq, na kwamba kipaumbele cha sasa kinapaswa kutolewa kwa mapambano dhidi ya Kundi la IS.

    Naye waziri mkuu wa Iraq Bw Haider al-Abadi amesema serikali kuu ya Iraq imekataa pendekezo lililotolewa na jimbo la wakurdi kuhusu kusitisha matokeo ya kura za maoni. Amesisitiza kwamba serikali yake itakubali tu kama matokeo ya kura hizo yafutwe, wala sio kusitishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako