• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu wawili wafariki kutokana na mvua kubwa iliyonyesha Dar es Salaam

    (GMT+08:00) 2017-10-27 09:26:20

    Watu wasiopungua wawili wamefariki dunia na wengine mamia wamepoteza nyumba zao baada ya mvua mkubwa kunyesha kwa zaidi ya saa 24 mjini Dar es Salaam, Tanzania.

    Mvua hiyo pia imeharibu miundo mbinu ikiwemo barabara na madaraja, na kukwamisha shughuli za biashara.

    Kamanda wa polisi wa Dar es salaam Bw Lazaro Mambosasa, amesema watu wawili wamefariki baada ya kusombwa na mafuriko, na nyumba zaidi 70 zimeharibika kutokana na mvua. Ameongeza kuwa baadhi ya waathirika wamehifadhiwa katika shule na makanisa kwa muda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako