• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ni hulka ya binadamu kuogopa nyoka na buibui

  (GMT+08:00) 2017-10-27 19:41:57

  Wanasayansi wa Ulaya wamefanya majaribio na kugundua kuwa ni hulka ya binadamu kuogopa nyoka au buibui.

  Katika jamii ya kisasa watu wengi hawajawahi kuona nyoka au buibui wenye sumu, lakini bado kuna watu wengi wanaoogopa nyoka na buibui. Baadhi ya wanasayansi wanasema binadamu wanaokua wamejifunza kuogopa wanyama hatari, lakini baadhi wanasema hofu hiyo ni hulka.

  Wanasayansi wa idara mbalimbali ikiwemo taasisi ya sayansi ya ufahamu na ubongo wa binadamu ya Max Planck ya Ujerumani wamefanya majaribio kuonesha picha mbalimbali ikiwemo maua, samaki, buibui au nyoka kwa watoto wachanga wenye umri wa miezi 6. Matokeo yanaonesha kuwa mboni za macho yao zilipanuka kwa kiasi kikubwa wakati walipoona picha za buibui na nyoka.

  Watafiti wamesema wakati mwanga haubadiliki, kupanuka kwa mboni za macho ni ishara ya kukabiliwa na shinikizo, yaani watoto wachanga wanaogopa buibui na nyoka bila kufundishwa.

  Picha za dubu na kiboko hazitasababisha hofu ya watoto wachanga, kwa sababu mamalia hao waliishi na mababu za binadamu kwa muda mfupi, na binadamu hawajapata hulka ya kuwaogopa wanyama hao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako