• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kundi la waasi kutoka Uganda ADF lafanya mashambulizi mawili tofauti mjini Beni DRC

  (GMT+08:00) 2017-10-27 20:08:28

  Licha Ya juhudi zinazoendeshwa na serikali Ya jamhuri Ya kidemokrasia Ya kongo kuhakikisha eneo la mashariki mwa nchi hiyo linakuwa salama, makundi korofi bado yanaendelea kuhatarisha usalama wa watu na mali zao. Jana kundi la waasi kutoka Uganda ADF lilifanya mashambulizi mawili tofauti mjini Beni. Moja kwenye Hospitali, na la pili kwenye kambi ya jeshi maeneo ya mjini, na kuleta taharuki iliyofanya baadhi ya watu kukimbia makazi yao. Mwandishi wetu MSEKE DIDE anatuandalia ripoti ifuatayo :

  Shambulizi hili lilifanyika mwendo wa saa kumi na moja za jioni majira ya Afrika ya kati, saa chache baada ya balozi wa Marekani kwenye umoja wa mataifa Bibi Nick Haley kuwasili mjini Goma, kujionea na kujadili hali ya amani na usalama nchini DRC. Milio ya silaha nyepesi na nzito ilisikika katika sehemu ya kati ya mji wa Beni, ni ndani ya kata la Boikene upande wa KIPRIANI na MATETE mkoani Kivu ya Kaskazini . Kutokana na mtafaruku wakazi walikuwa wakikimbia bila kuangalia nyuma, na wengine walijikuta wakipotezana na watoto wao, kama wanavyoeleza hapa.

  Imetajwa kuwa watu tano wameuawa wakiwemo askari watatu wa jeshi la serikali na raia wawili. Serikali bado haijatoa idadi kamili ya watu waliouawa au kujeruhiwa, licha ya Mea wa mji wa Beni, aliyetangaza kuwa ,jeshi la serikali limefanikiwa kuwafukuza waasi wa ADF, kwa kushirikiana na Jeshi la kimataifa, haswa kikosi maalumu cha uingiliaji wa haraka FIB chenye askari kutoka Afrika Kusini na Tanzania. Viongozi wa serikali watoa mwito kwa raia kuwa na utulivu.

  Ikumbukwe kwamba sio mara ya kwanza kwa tukio kama hili kutokea, lakini wasiwasi ni kuwa ni mashambulizi mawili yametokea ndani ya muda mfupi katika maeneo tofauti. Mapema alhamisi Hospitali moja inayojulikana kwa jina la CME NYANKUNDE, ilishambuliwa na kushuhudiwa uporaji wa vifaa vya kisasa vya matibabu, dawa na pesa taslimu, madaktari na wagonjwa walikimbia, baada ya walinzi kushambuliwa na kupigwa. Hakuna anayejua hasa ni nani anahusika na tukio hilo. Nimezuru eneo la tukio na kukutana na wahanga waliokuwa kwenye vitanda vya wagonjwa, hawakusita kuongelea mkasa wenyewe.

  "Mimi si mgonjwa bali nachunga mgonjwa.

  Majambazi walipoingoia walianza kusukuma mlango,nasi tukazuia mlango ;lakini mwengine wao alibomowa vioo vya dirisha na kuingia ndani ;hata tukashindwa cha kufanya hadi walipoonza kupiga na kuomba pesa na simu"

  "Maana yake tumeteseka sana ten asana;licha ya kuwa mgonjwa kwa namna hii;wamenikokota kokota;wakiniomba pesa na simu za mkononi;wala hawakunijali hata kidogo"

  Mjumbe mkuu wa Hospitali hiyo mwuguzi EMMANUEL SIYABO YANDISHABO, kwa niaba ya jopo madaktari alikuwa na haya ya kusema.

  "Tumekuwa ni Message moja tu ;tunaomba kwa wakuu viongozi kuhakikisha kwamba tunapata amani ;kwa kuwa bila amani hatuwezi kuchapa kazi vilivyo.

  Inapofikia kwa hatuwa ya kuwapiga hata wagonjwa ;kwa kweli ni huzuni sana"

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako