• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran na IAEA watoa mwito kwa pande zote kuheshimu makubaliano ya nyuklia

    (GMT+08:00) 2017-10-30 09:02:32

    Maofisa wa Iran na mkuu wa Shirika la kimataifa la nishati ya atomiki IAEA Bw. Yukiya Amano, wametoa mwito kwa pande zote kutekeleza makubaliano ya kimataifa ya nyuklia yaliyofikiwa mwaka 2015.

    Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema nchi yake itaendelea kutekeleza makubaliano hayo kama Iran inanufaika na makubaliano hayo. Akiongea na Bw Amano mjini Tehran, Rais Rouhani amesema nchi yake haitakuwa ya kwanza kujitoa kwenye makubaliano hayo, iliyosaini pamoja na nchi nyingine sita.

    Mapema mwezi Rais Donald Trump alisema Marekani haitaidhinisha rasmi kuwa Iran inatekeleza makubaliano ya nyuklia, na imetaka kuwe na ukaguzi kwenye vituo vya kijeshi vya Iran, jambo ambalo Iran imekataa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako