• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Sudan Kusini kufanya ziara Sudan

    (GMT+08:00) 2017-10-30 09:12:54

    Ikulu ya Sudan imesema, rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan Kusini atafanya ziara ya siku mbili nchini Sudan kuanzia Jumatano wiki hii.

    Kwenye ziara yake rais Kiir atafanya mazungumzo na mwenzake wa Sudan Omar al-Bashir, ambapo watashuhudia kusainiwa kwa makubaliano kadhaa kati ya nchi hizo mbili.

    Kwa mujibu wa mpango, mawaziri wa nchi hizo mbili pia watafanya mazungumzo katika kipindi cha ziara hiyo.

    Sudan na Sudan Kusini zimeshindwa kutekeleza makubaliano yaliyosainiwa mwezi Septemba mwaka 2012 huko Addis Ababa kwa usuluhishi wa Umoja wa Afrika. Makubaliano hayo ni pamoja na yanayohusu usalama, hadhi ya wananchi, mpaka, uchumi na mambo mengine yanayohusu mafuta na biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako