• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yasisitiza ahadi yake ya kufanya ushirikiano wa kiujenzi na Marekani

    (GMT+08:00) 2017-10-30 09:36:14

    Sudan imesisitiza ahadi yake ya kufanya ushirikiano ya kiujenzi kati yake na Marekani.

    Naibu waziri wa mambo ya nje wa Sudan Bw. Abdul-Ghani Al-Naneem amesema hayo alipokutana na bibi Sandra Oudkirk, kaimu naibu katibu wa idara inayoshughulikia mapambano dhidi ya matishio ya kifedha na vikwazo kwenye Ofisi ya mambo ya uchumi na biashara ya Marekani, ambaye yuko ziarani nchini Sudan.

    Bw. Al-Naneem amesema Sudan iko tayari kujenga utaratibu wa kiutendaji utakaosaidia kuanzishwa kwa ushirikiano kwa ajili ya amani na maendeleo, utakaozinufaisha nchi hizo mbili.

    Kwa upande wa ofisa wa Marekani, Bibi Oudkirik ameeleza kuwa Marekani pia iko tayari kupanua ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na Sudan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako