• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa umoja wa mataifa alitaka baraza la usalama liunge mkono kikosi cha Sahel

    (GMT+08:00) 2017-10-31 08:42:09

    Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bw Antonio Guterres amelitaka baraza la usalama kuwa na mipango kabambe ya kuunda kikosi cha pamoja katika eneo la Sahel.

    Akiongea kwenye mkutano wa mawaziri wa kundi la nchi tano za Sahel linaloundwa na Mali, Niger, Burkina Faso, Chad na Mauritania, amesema uungaji mkono wa kisasa, vifaa na kiutendaji unaoendana na changamoto za sasa ni muhimu.

    Bw Guterres amesema hali ya umaskini, kukosa maendeleo na mabadiliko ya hali ya hewa, vimechochea misukosuko ya kibinadamu na usalama katika eneo hilo. Ametaja udhaifu wa idara za eneo hilo, na kupuuzwa kwa baadhi ya makundi ya watu kwenye jamii kunatumiwa na magaidi. Pear amesema udhaifu kwenye usimamizi wa mipaka unafanya magendo ya binadamu, dawa za kulevya na silaha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako