• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbunge wa Chama cha mapinduzi cha Tanzania atangaza kuhamia chama cha upinzani

    (GMT+08:00) 2017-10-31 08:42:48

    Mbunge wa jimbo la Singida Kaskazini kwa tiketi ya chama cha mapinduzi Bw Lazalo Nyalandu ametangaza kujitoa kwenye chama cha mapinduzi na kujiunga na chama kikubwa cha upinzani CHADEMA.

    Bw Nyalandu ametangaza kujitoa kwenye chama hicho kwenye barua aliyomwandikia spika wa bunge la Tanzania Bw. Job Ndugai. Bw Nyalandu alikuwa mbunge wa jimbo la Singida Kaskazini kwa miaka 17 tangu mwaka 2000, na kuwa na nyadhifa mbalimbali ndani ya chama.

    Bw. Nyalandu aliyewahi kuwa waziri wa maliasili na utalii, amesema kujitoa kwake CCM kunatokana na kutoridhishwa na jinsi kinavyoendesha utawala na hakuna mipaka kati ya mihimili ya dola.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako