• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwendesha mashtaka wa Hispania atangaza hatua za kisheria dhidi ya viongozi wa zamani wa jimbo la Catalonia

    (GMT+08:00) 2017-10-31 09:16:57

    Mwendesha mashtaka wa Serikali ya Hispania Bw. Jose Manuel Maza ametangaza kuwa kiongozi wa zamani wa jimbo la Catalonia Bw. Carles Puigdemont na maofisa wa serikali yake ambao walitangaza uhuru wa jimbo hilo watafanyiwa uchunguzi kutokana na mfululizo wa uhalifu ikiwa ni pamoja na uasi, uchochezi wa vurugu, matumizi mabaya ya fedha za umma.

    Bw. Puigdemont na serikali yake walifukuzwa kazi Ijumaa na waziri mkuu wa Hispania Bw. Mariano Rajoy kwa mujibu wa kifungu cha 155 cha Katiba ya Hispania, ambacho kimesimamisha hatua ya kujitangazia uhuru kwa jimbo la Catalonia na kukabidhi udhibiti wa taasisi muhimu za jimbo hilo kwa serikali kuu kabla ya uchaguzi mpya utakaofanyika Desemba 21.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako