• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matokeo ya mechi za ligi ya mabingwa barani Ulaya (UEFA)

    (GMT+08:00) 2017-11-01 08:23:53
    Manchester United wakiwa nyumbani katika dimba la Old Trafford imefanikiwa kuinyuka Benfica 2-0. Anthony Martial alikuwa tishio kwenye mchezo huo alikosa mkwaju wa penalti baada ya kuangushwa eneo la hatari. Matokeo ya mechi zingine, Chelsea imepoteza baada ya kukubali kipigo cha 3-0 toka kwa AS Roma.

    PSG wao wameifanyia mauaji Anderlecht kwa kuichapa 5-0 huku Neymar akifunga goli moja kati ya matano.

    Barcelona wao wamesubirishwa kuiona 16 bora ya michuano hiyo baada ya kulazimishwa suluhu ya 0-0 na Olympiakos, huku Sporting CP nao wakiilazimisha Juventus sare ya 1-1.

    Matokeo mengine, Atletico Madrid wameendelea kukumbwa na mzimu wa sara baada ya kutoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Quarabag FK. Bayern Munich yenyewe imeifunga Celtic 2-1.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako