• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China asisitiza kukumbuka historia ya chama na kufanya juhudi bila kusita kutimiza majukumu yake

  (GMT+08:00) 2017-11-01 09:29:53

  Ni wiki moja imepita tangu kufungwa kwa Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha kikomunisti cha China, katibu mkuu wa Kamati kuu ya Chama Bw. Xi Jinping akiongoza wajumbe wa kudumu wa Ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama wamefanya ziara katika mji wa Shanghai, na Jiaxing mkoani Zhejiang, kutoa heshima mahali ulipofanyika Mkutano mkuu wa kwanza wa chama, wakikumbuka historia ya chama cha kikomunisti cha China, kiapo cha kujiunga na chama, na kutangaza imani imara ya kisiasa ya awamu mpya ya viongozi wa kamati kuu.

  Bw. Xi Jinping amesisitiza kutosahau imani ya awali, kukumbuka majukumu ya chama na kufanya juhudi bila kusita. Amesema kama wanachama na watu wa makabila mbalimbali wa China watashikamana na kufanya kazi kwa bidii, lengo la kustawisha upya taifa la China litapata mafanikio.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako