• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan na Sudan Kusini zakubaliana kupanga upya jeshi nje ya eneo lisilokuwa na shughuli za kijeshi

    (GMT+08:00) 2017-11-01 09:34:30

    Waziri wa ulinzi wa Sudan Bw Awad Ibn Auf na mwenzake wa Sudan Kusini Bw Kuol Manyang Juuk wamesaini makubaliano ya kupanga upya vikosi vyao nje ya eneo lisilokuwa na shughuli za kijeshi katika eneo la mpakani, kwenye mkutano kati ya nchi hizo mbili uliofanyika jana mjini Khartoum.

    Msemaji wa jeshi la Sudan Ahmed Khalifa Al-Shami amesema, licha ya hayo pande hizo mbili pia zimekubaliana kuanzisha tena kamati ya pamoja ya siasa na usalama na kituo cha pamoja cha usimamizi wa eneo la mpaka. Pia amesema hatua hizo zitatekelezwa ndani ya mwezi mmoja na kamati hiyo itakutana mjini Juba mwezi wa Januari mwakani.

    Habari zinasema, nchi hizo mbili zimeshindwa kutekeleza kikamilifu makubaliano ya ushirikiano yaliyosainiwa mwaka 2012 mjini Addis Ababa, Ethiopia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako