• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idara ya mawasiliano na nje ya Kamati kuu ya CPC yawajulisha mabalozi wa nchi za kigeni moyo wa mkutano mkuu wa 19

    (GMT+08:00) 2017-11-01 18:19:48

    Idara ya mawasiliano na nje ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC imefanya mkutano unaolenga kuwajulisha maofisa wa kibalozi wa nchi za kigeni nchini China na wajumbe wa vyama vya kibiashara na mashirika, moyo wa mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha kikomunisti cha China. Maofisa waandamizi 260 hivi wa kibalozi kutoka nchi zaidi ya 150 wakiwemo mabalozi zaidi ya 90 wamehudhuria mkutano huo.

    Naibu mkuu wa wa idara hiyo Bw. Guo Yezhou amesema, huu ni mkutano muhimu sana kufanyika katika kipindi muhimu ambapo China inatimiza jamii yenye maisha bora kwa pande zote na Ujamaa wenye umaalumu wa China kuingia katika kipindi kipya. Pia amejulisha hali za mkutano huo katika upande wa maneno muhimu yakiwemo mawazo mapya, mafanikio mapya, kipindi kipya, safari mpya, matakwa mapya na mchango mpya.

    Kwenye mkutano huo, Bw. Guo pia alibadilishana maoni na mabalozi kutoka Tanzania, Uzbekistan na Romania kuhusu masuala ya ushirikiano na nchi jirani na maendeleo ya sekta mbalimbali katika kipindi kipya ya China yaliyomo kwenye ripoti iliyotolewa na rais Xi Jinping katika mkutano mkuu wa 19 wa chama cha CPC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako