• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Korea Kusini asema mapigano hayatatokea kwenye peninsula ya Korea katika hali yoyote

    (GMT+08:00) 2017-11-01 18:42:10

    Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini ametoa hotuba kwenye kikao cha bunge akieleza msimamo wa kimsingi wa serikali yake kuhusu utatuzi wa suala la nyuklia la Korea Kaskazini na kutimiza amani ya peninsula ya Korea.

    Rais Moon amesema, peninsula hiyo ni eneo wanaloishi wananchi wa Korea Kusini, hivyo nchi hiyo inatakiwa kulinda amani na usalama wa peninsula hiyo. Ameongeza kuwa lengo lao kuu ni kutimiza amani ya peninsula hiyo, na katika hali yoyote mapigano hayatatokea. Mtu yeyote haruhusiwi kufanya vitendo vya kimabavu bila ya kupata ruhusa ya Korea Kusini.

    Pia amesema, Korea Kusini haitairuhusu Korea Kaskazini kuendeleza silaha za nyuklia, na nchi yake pia haitaendeleza au kumiliki silaha hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako