Wakulima wa matunda na mboga Zanzibar wamehimizwa kuzingatia ubora na mahitaji ya masoko.
Meneja wa mradi wa matunda na mboga nchini Tanzania Mdachi Bakari,wakati akizungumza na wakulima hao visiwani Zanzibar katika mkutano ulioandaliwa na shirika la kimataifa la kujitolea lenye lengo la kumaliza umasikini (VS0) alisema wakulima ni vyema wakulima wafahamu umuhimu wa ubora na mahitaji ya soko ili kupata bei nzuri kwa bidhaa zao.
Afisa wa masoko na ujasiriamali kutoka shirika la kimataifa la kujitolea kupunguza umasikini (VSO) Chris Takyuka amewahimiza wakulima hao kuwekeza zaidi katika kilimo cha matunda na mboga kwa kuwa kilimo hicho kina faida zaidi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |