• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya madaktari wa China waaanza kutoa matibabu bila malipo nchini Rwanda

    (GMT+08:00) 2017-11-02 09:22:35

    Timu ya 18 ya madaktari wa China wameanza kutoa matibabu bila malipo kwa muda wa wiki moja katika eneo la Kibungo, Rwanda.

    Mkuu wa kituo cha afya cha Kibungo Bibi Eugenie Imurinde amesema, ni vigumu kwa wagonjwa wengi wa eneo hilo hasa wanaoishi maeneo ya mbali kupata matibabu. Amewashukuru madaktari China kutoa matibabu bila malipo kwa wagonjwa.

    Kwa upande wake, mkuu wa timu hiyo Bw. Lu Jun amesema, kutoa matibabu bila malipo ni kazi muhimu kwa timu ya madaktari wa China. Timu hiyo imetoa dawa za malaria, homa na magonjwa ya wanawake kwa kituo hicho ili kuwasaidia wakazi wa huko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako