• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kundi la waangalizi wa uchaguzi wa Kenya latoa mwito wa kufanyiwa mabadiliko makubwa kwa sheria ya uchaguzi Kenya

    (GMT+08:00) 2017-11-02 09:33:28

    Kundi la waangalizi wenyeji wa uchaguzi wa Kenya, limetoa mwito wa kufanyika kwa mabadiliko makubwa kwenye sheria ya uchaguzi ya Kenya ili kuondoa dosari zilizojitokeza kwenye uchaguzi huo.

    Mwenyekiti wa kamati ya kundi la waangalizi wa uchaguzi Bibi Regina Opondo amewaambia waandishi wa habari mjini Nairobi kuwa mchakato wa kutunga sheria mpya ya uchaguzi inatakiwa kuwahusisha wadau wengi iwezekanavyo.

    Bibi Opondo amesema ukaguzi wao umegundua kuwa tume ya uchaguzi ya Kenya imeshindwa kuhakikisha usafi wa daftari ya orodha ya wapiga kura, taratibu za gharama za uchaguzi sio za haki na kutaka kuwe na utaratibu wa kuwasimamia wagombea kutii katiba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako