• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marekani yapitisha tiba ya jeni ya kwanza

  (GMT+08:00) 2017-11-02 20:31:44

  Serikali ya Marekani imepitisha tiba ya kubadilisha seli za kinga maradhi ya mwili wa wagonjwa ili kutibu ugonjwa wa damu ambayo hii ni tiba ya jeni ya kwanza inayoidhinishwa na Marekani. Wataalamu wanaona kuwa tiba hiyo imefungua ukurasa mpya wa tiba ya saratani.

  Idara ya usimamizi wa chakula na dawa ya Marekani imetoa taarifa ikisema, tiba mpya ya kampuni ya Novartis ya Uswisi imeidhinishwa, ambayo itatumiwa kutibu wagonjwa wa damu chini ya miaka 25. Imeongeza kuwa hii ni hatua ya kihistoria itakayofungua ukurasa wa kutibu saratani na maradhi mengine makali ya kuharibu maisha.

  Tiba hiyo mpya ni tiba ya CAR-T inayoendelezwa katika miaka ya hivi karibuni. Tiba hiyo inakusanya seli za T zinazotoa mchango mkubwa katika mchakato wa kinga maradhi, halafu kuzihariri, ili kuzifanya seli hizo za T kuweza kutambua na kushambulia seli za saratani.

  Jaribio lililowashirikisha wagonjwa 63 limeonesha kuwa baada ya kupatiwa tiba hiyo kwa miezi 3, hali ya ugonjwa ya asilimia 83 ya wagonjwa imepona kwa kiasi. Baada ya kupatiwa tiba kwa mwaka mmoja, kiwango cha kutokea tena kwa ugonjwa huo ni asilimia 64 huku kiwango cha kuishi kikiwa asilimia 79.

  Mkurugenzi wa idara hiyo amesema, kuhariri seli za wagonjwa na kuzitumia kuua saratani, kunamaanisha tumeingia katika kipindi kipya cha ubunifu wa matibabu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako