• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Samata, Onyango na Olunga kuwania tuzo za mchezaji bora barani Afrika 2017

    (GMT+08:00) 2017-11-03 08:30:48

    Denis Onyango wa Uganda, Mbwana Samata wa Tanzania na Micheal Olunga wa Kenya wameteuliwa kuwania taji la mchezaji bora barani Afrika 2017. Watatu hao ndio wachezaji kutoka eneo la Afrika mashariki ambao wameorodheshwa katika orodha ya wachezaji 30 iliyotolewa na shirikisho la soka barani Afrika Caf.

    Mshindi ataamuliwa kupitia kura za makocha, wakurugenzi wa kiufundi na miungano ya kitaifa inayoshirikiana na Caf, wanachama wa kamati ya kiufundi na maendeleo ya Caf pamoja na jopo la wanahabari.

    Winga wa Algeria na Leicester Riyad Mahrez ndio bingwa mtetezi wa taji hilo baada ya kumshinda Pierre Emerick Aubameyang na Sadio Mane. Sherehe hiyo itafanyika Alhamisi ya tarehe 4 2018 mjini Accra, Ghana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako