• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wauguzi wa Kenya wamaliza mgomo uliodumu miezi 5

    (GMT+08:00) 2017-11-03 09:22:24

    Wauguzi wa Kenya wamemaliza mgomo uliodumu kwa miezi 5 baada ya kufikia makubaliano na baraza la magavana la nchi hiyo, CoG.

    Katibu mkuu wa jumuiya ya wauguzi wa Kenya Bw Seth Panyako amesema makubaliano hayo yatatekelezwa kikamilifu ndani ya siku 30 na kuwataka wauguzi warudi kazini kuanzia leo.

    Amesema wafanyakazi wa afya wataongezewa marupurupu yao. Pande mbili pia zimekubaliana kuwa kesi zote zinazohusiana na mgomo huo kwenye mahakamani zitafutwa.

    Wauguzi wa Kenya walianza mgomo mwezi Juni na kusababisha kusitishwa kwa huduma za afya nchini humo, huku wagonjwa wakilazimika kwenda hospitali binafsi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako