• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania yaeleza mafanikio ya rais Magufuli yaliyopatikana katika miaka miwili iliyopita

    (GMT+08:00) 2017-11-06 10:06:01

    Serikali ya Tanzania imeeleza mafanikio ya rais John Magufuli yaliyopatikana tangu alipoingia madarakani miaka miwili iliyopita.

    Mkurugenzi mkuu wa idara ya huduma ya habari Bw Hassan Abbas amesema mafanikio makubwa ni kurudisha nidhamu kwa watumishi wa umma hali iliyosaidia kuboresha utoaji wa huduma. Pia kumekuwa na udhibiti wa matumizi ya fedha za serikali, na kuhakikisha fedha kwa ajili ya miradi ya serikali zinatumika vizuri. Ameongeza kuwa wafanyakazi hewa na wale wenye vyeti feki wasiopungua elfu 30 wamefukuzwa kazi.

    Bw. Abbas amesema rais Magufuli ameimarisha mapambano dhidi ya ufisadi, na kuanzisha mahakama maalumu dhidi ya maofisa wanaohusika na ufisadi. Pia ametaja mafanikio kwenye sekta za uhifadhi wa maliasili, kuongezeka kwa uwezo wa kujitegemea na elimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako