• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu 20 wameuawa kwenye mauaji yaliyotokea kanisani katika jimbo la Texas

  (GMT+08:00) 2017-11-06 15:56:03

   

  Watu 20 wameuawa kwa kupigwa risasi kanisani katika jimbo la Texas nchini Marekani, baada ya mtu mwenye bunduki kuingia kanisani na kuwafyatulia risasi. Watu wengine wanane wamejeruhiwa katika tukio hilo na sasa wanapatiwa matibabu.

  Tukio hilo limetokea katika kanisa la Baptist umbali wa kilometa 35 kutoka mji wa San Antonio. Muuaji ambaye alikimbia baada ya tukio, aliuawa kwa kupigwa risasi kilometa tisa kutoka kwenye eneo la tukio, baada ya kuzingirwa na wanausalama.

  Rais Donald Trump wa Marekani ambaye yuko ziarani nchini Japan amesema anafuatilia kwa karibu tukio hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako