• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jinsi kitambi kinavyoongeza hatari ya saratani

  (GMT+08:00) 2017-11-06 15:57:19

  Kama tunavyofahamu, unene unaweza kuongeza hatari ya saratani, hasa mafuta ya tumboni yanaleta hatari kubwa zaidi. Utafiti mpya umeonesha kuwa mafuta tumboni yanaweza kuzalisha protini inayohimiza seli za kawaida kuwa seli za saratani.

  Unene umethibitishwa kuhusika na saratani za aina mbalimbali, ikiwemo saratani ya matiti na saratani ya utumbo mpana. Watafiti wa chuo kikuu cha Michigan cha Marekani wamesema, katika upande wa tathmini ya saratani, kutathmini kiwango cha mafuta tumboni ni sahihi zaidi ikilinganishwa na kutathmini hali ya unene ya mwili.

  Timu hiyo ya utafiti imetoa ripoti ikisema, wamewalisha panya chakula chenye mafuta mengi na kufanya utafiti. Wakagundua kuwa mafuta tumboni yamezalisha idadi kubwa ya protini maalumu ambayo inazifanya seli za kawaida kuwa dhaifu na kubadilika kuwa seli za saratani. Yakilinganishwa na mafuta ya chini ya ngozi, mafuta ndani ya maini yanaweza kuzalisha protini nyingi zaidi ya aina hiyo.

  Baada ya hapo, watafiti wameweka mafuta yaliyokusanywa katika mwili wa binadamu kwenye mwili wa panya. Matokeo yameonesha kuwa mafuta yanazalisha protini nyingi zaidi ya aina hiyo, seli nyingi zaidi zinakuwa seli za saratani.

  Utafiti umependekeza kuwa, watu wanatakiwa kutilia maanani mafuta yaliyomo ndani ya tumbo, kudhibiti kitambi kupitia udhibiti wa chakula na mazoezi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako