• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yarusha satellite mbili za uongozaji za Beidou-3 katika anga za juu

  (GMT+08:00) 2017-11-06 16:41:33

  China imerusha satellite mbili za Beidou-3 katika anga za juu kwa kutumia roketi moja ya uchukuzi ili kuunga mkono mtandao wa kimataifa wa mfumo wa uongozaji wa satellite za Beidou.

  Satellite hizo mbili zilirushwa na roketi ya Changzheng-3 ambayo iliruka saa 1:45 jioni ya Jumapili kutoka Kituo cha kurushia satellite cha Xichang katika mkoa wa kusini magharibi wa Sichuan.

  Hizi ni satellite mbili za kwanza za Beidou-3 kurushwa na China, hatua ambayo inalenga kufanya mfumo wa uongozaji wa satellite za Beidou wa China kutoa huduma kwa dunia mapema iwezekanavyo. Mfumo huo ni miundombinu muhimu ya China katika anga za juu. Mradi wa Beidou-3 ulizinduliwa rasmi mwaka 2009, na katika miaka minane iliyopita China imemiliki teknolojia kuu na kumaliza majaribio yake ardhini. Msanifu mkuu wa Mfumo wa Uongozaji wa satellite za Beidou Yang Changfeng anasema,

  "Kutoka Beidou-1, Beidou-2 hadi Beidou-3 ya sasa, mfumo wa Beidou umeboreshwa hatua kwa hatua. Hii inatokana na maendeleo ya sekta ya uongozaji ya satellite duniani, na China inatafuta na kujenga mfumo wa maendeleo wa uongozaji wa satellite wenye umaalum wa kichina."

  Akitoa maoni yake kuhusu satellite mbili za Beidou-3 zilizorushwa jana, naibu msanifu mkuu wa mradi wa Beidou-3 Xie Jun anasema,

  "Satellite hizi mbili zimeboreshwa sana katika sekta mbalimbali zikilinganishwa na Beidou-2, na zinaweza kushirikiana vizuri na mifumo mingine ya uongozaji ikiwemo GPS ya Marekani na GLONAS ya Russia."

  China inapanga kurusha satellite 18 za Beidou-3 kabla ya mwishoni mwa mwaka 2018 ili kupanua huduma za Beidou kwa nchi zilizo katika Ukanda Mmoja, Njia Moja. Na inatarajiwa kuwa hadi kufikia mwaka 2020 mfumo wa satellite za uongozaji za Beidou utatumiwa kimataifa, na utakuwa na satellite zaidi ya 30.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako