• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Afghanistan lawaua waasi 14 kwenye mkoa wa Helmand

    (GMT+08:00) 2017-11-06 18:58:49

    Wizara ya ulinzi ya Afghanistan imesema, waasi 14 wameuawa na wengine 15 kujeruhiwa kwenye operesheni iliyofanywa na jeshi la Afghanistan huko Nad Ali mkoa wa Helmand, kusini mwa nchi hiyo.

    Ikitangaza kupitia Twitter, Wizara hiyo imesema, magari matano na pikipiki 5 pia zimeharibiwa kwenye opresheni hiyo.

    Helmand ndio ngome kuu ya kundi la Taliban.

    Vikosi vya usalama vya Afghanistan vimeimarisha operesheni ya kijeshi dhidi ya wapiganaji, huku wapiganaji wa kundi la Taliban na kundi la IS wakijaribu kutawala eneo zaidi na kuimarisha nafasi zao kabla ya majira ya baridi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako